Tundu Lissu: Nafuatiliwa na Usalama wa Taifa kwa wiki 3 sasa



  

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amedai kwamba anafuatiliwa na watu anaowashuku kuwa ni Maafisa Usalama, katika kipindi cha wiki tatu mfululizo. Hata hivyo hajabainisha sababu ya kufuatiliwa kwake.
Lissu ameyaeleza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari, na kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kuwaeleza wakubwa wao kuhusu kuwaelekeza watumishi hao kupambana na wahalifu badala ya kutumia rasilimali za nchi kufuatilia raia wasio na hatia.
Lissu amedai kuwa, watumishi hao wanapaswa kutumia vema rasilimali za nchi kwa kupambana na wahalifu badala ya kuhangaika na wananchi wanaotimiza wajibu wao kikatiba katika kuwawajibisha baadhi ya viongozi wasiotimiza wajibu wao.
“Mkuu wa TISS au IGP wale vijana mliowatuma wiki tatu mfululizo kunifuata kila nilipo, niliowakaba Kanisani St. Peter, muwaambie wakubwa wawaelekeze watumishi wao kutumia muda na rasilimali za nchi kupambana na wahalifu na si kuhangaika na raia wanaotimiza wajibu wao kikatiba kuwawajibisha viongozi serikalini,” amesema

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.