MAMBO YANAYOPUNGUZA UWEZO WA BETRI NA MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO HILO.



Betri ni kifaa muhimu sana kwenye Kompyuta ambacho mara nyingi ndicho hutunza umeme wa ziada(backup), na mara zote ili betri iweze kuchaji lazima mzunguko wa umeme upitie kwenye ubao mama(motherboard) na kusambaa kuelekea kwenye Betri kitendo ambacho huchukua muda mfupi sana kukamilika.
Kwa uzoefu uliopo ni kwamba betri huundwa na Seli ambazo hujipanga sambamba ili kukamilisha mfumo mzima wa umeme. Na kiwango cha volti kwenye kila Seli huwa ni 1.5v.
Na kwa kawaida kiwango cha betri kuisha muda wake (life style) huwa ni miezi 10-24, hivyo ukiona betri yako haijafika hapo elewa kuwa kuna matumizi mabaya ya betri yako, pia ukiona miezi hiyo imefika yaani miaka miwili yafaa ukabadilisha betri yako.

Hebu kwa leo tuangalie kwa mapana sana kuhusu Mambo yanayosababisha betri kuhusu betri kuharibika n ahata kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
         
               MATUMIZI MABAYA YA BETRI
Limekuwa ni tatizo kubwa sana ambapo unakuta mtu anatumia Kompyuta yake lakini anashindwa kuwa muangalifu na umakini wa hali ya juu. Katika kipengele hiki tutaangalia kwa mapana kuhusu,
- Kuchaji Kompyuta bila kutoa Adapter baada ya Kompyuta kujaa, wakati watu wanatumia Kompyuta zao huweka “charger” (Adapter), na wakati Kompyuta imefikia kiwango cha 100% huku imeandika “Full charged” bado huendelea kuweka adapter bila kuitoa, kitendo hicho kwa kiwango cha hali ya juu husababisha Kupungua kiwango cha kuishi kwa betri yako n ahata kupelekea kufa kabisa. Hivyo unashauriwa ukiona betri imejaa ni vyema ukatoa Adapter, tumia mpaka chaji iishe na ndipo uanze kuchaji upya.
Usipende kuacha ADAPTER yako kwenye Kompyuta kwa muda mrefu wakati imeishajaa.
- Kutumia ADAPTER ambayo haiendani na “model” ya Kompyuta yako, ni kosa kubwa kutumia Mfano Adapter ya Kompyuta ya dell kuchaji Kompyuta ya HP, sawa inaweza ikawa inachaji lakini kumbe unaandaa mazingira ya kuua betri yako. Ndio maana tunashauri kuangalia “Model” ya Kompyuta yako kabla ya kununua kifaa chochote kipya kwa ajili ya Kompyuta yako.
- Kuwasha/ kutumia software ambazo hata wakati huo hazina umuhimu, yawezekana unapokuwa unatumia Kompyuta yako ukawasha hizo “software” mfano, “Bluetooth” wi-fi, n.k. Inashauriwa unapomaliza kutumia hizo software ni vyema ukazima maana nazo kwa kiwango Fulani husababisha betri yako kupungua nguvu.
- Kuweka baadhi ya vifaa kwa kiwango cha hali ya juu kwenye Kompyuta yako, mfano utakuta mtu anatumia Kompyuta yake Kuchaji simu, powerbank, wakati huo ameweka “external Hard drive”, kitendo hicho hupunguza pia kiwango cha utendaji wa betri yako.
Katika maelezo hapo juu tumeeleza kwa kina mambo yanayofanyika na pia tumetoa suluhisho la hayo yote ili uweze kuweka betri yako kwa kiwangob salama.
 Pia zingatia kufanya yafuatayo ili betri yako iweze kuishi muda mrefu
- Epuka “ku-sleep” au “ku-hibernate” Kompyuta yako, maana pia huwa ni chanzo cha betri kuharibika.
- Pia uwe na mazoea ya kuseti alama iliyoandikwa “Balanced” kwenye batri yako pale inapokuwa unachaji
- Pia jitahidi sana kuweka Mwanga hafifu hasa unapokuwa sehemu kama ofisini, sehemu ambayo unaona kuna uwezekano wa kupunguza mwanga, maana pia mwanga mwingi kwa kiwango kingine husababisha betri kupungua nguvu.

N.B Kwa kiwango kilekile unavyotunza betri ya Kompyuta yako, unaweza kukitumia kutunza betri ya Simu yako, nayo ikapata kuishi kwa muda mrefu sana.
 Image result for LAPTOP


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.