Ibrahimovic akubaliana na mashetani wekundu


Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic.

Ibrahimovic alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti alilolipata tangu Aprili 28.
Mchezaji huyo wa Old Trafford aliifungia timu hiyo jumla ya mabao 28 katika michezo 46 aliyocheza msimu uliyopita.
Mara baada ya kusajiliwa Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 amesema “Nimerudi United kumalizia kile nilichokianza”, amesema Zlatan Ibrahimovic.
“Kamwe siwezi kuondoka katika dimba la Old Trafford na kwa sasa nitatumia muda wangu wakutosha ilikujiweka sawa”.
Mchezaji huyo sasa atakuwa akivaa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Wayne Rooney aliyejiunga na Everton.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.