NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA, TUMA MAOMBI KABLA YA TAREHE 28 AUGUST 2017
HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA
TANGAZO LA NAFASI YA KAZIHalmashauri ya Jiji la Mwanza imepokea Kibali cha ajira mpya chenye
kumb.Na.TA 170/359/01/22 cha tarehe 20/07/2017 kutoka kwa Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.Kutokana na kibali hicho,
Mkurugenzi wa Jiji anawatangazia waombaji wote wenye sifa kutuma maombi ya
nafasi hizo kwa kuzingatia vigezo na maelekezo yaliyo katika Tangazo hili:-
SIFA KWA UJUMLA:-
Mwombaji wa nafasi ya kazi anatakiwa:-
Awe Raia waTanzania
Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea
Awe na umri kati ya miaka 20-40
Awe na uwezo wa kutumia kompyuta.
Maombi yaambatane na vivuli vya vyeti vya shule na taaluma pamoja na
maelezo binafsi (CV).
Awe hajawahi kushtakiwa na kutiwa hatiani kwa makosa ya Jinai.
NAFASI ZA KAZI:-
1. Mtaa Executive II - (NAFASI 2)
KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA:-
Katibu wa Kamati ya Mtaa
Mtendaji Mkuu wa Mtaa
Mratibu wa utekelezaji wa sera na sheria zinazotekelezwa na Halmashauri
katika Mtaa.
Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu mipango ya Maendeleo katika Mtaa
Msimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogo pamoja na sheria nyingine
zinazotumika katika Mtaa.
Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.
Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa
njaa na umaskini katika Mtaa.
Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza
kumbukumbu za walipa kodi wote katika Mtaa.
Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa.
UWAJIBIKAJI:-
Afisa Mtendaji wa Mtaa atawajibika kwa Afisa Mtendaji wa Kata.
SIFA:-
Mwombaji awe na elimu ya Kidato cha Nne (IV) au (VI) Sita ambaye
amehitimu Stashahada (Diploma) katika Fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya
Jamii, Usimamizi wa Fedha na Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya jamii kutoka
Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA:-
Ngazi ya mshahara itakuwa TGS.C waombaji watakaofanikiwa kuajiriwa
wataanza na mshahara wa shilingi laki tano na ishirini na tano (Tsh. 525,000)
kwa mwezi .
2. DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 1
KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA II
Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote,
kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu
unaohitaji matengenezo.
Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari
Kuendesha gari ya abiria na malori
Kutunza na kuandika daftari la safari ‘’Log book’’ kwa O safari zote.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha kuhitimu Kidato cha Nne (IV) au (VI) Sita ,
mwenye leseni daraja la ‘’C’’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa
kuendesha magari na malori kwa muda usiopungua miaka (3) mitatu bila
kusababisha ajali, mwenye cheti cha majaribio ya ufundi Darajala II
NGAZI YA MSHAHARA:- TGOS – A shilingi laki tatu (300,000/=) kwa
mwezi.
3. KATIBU MAHSUSI III - NAFASI 5
KAZI NA MAJUKUMU YA KATIBU MAHSUSI III
Kuchapa barua taarifa na nyaraka za kawaida
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kuhudumiwa.
Kusaidia kutunza taarifa, kumbukumbu za matukio, miradi, wageni tarehe
za vikao na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu
chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake
na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa anapewa na wasaidizi
hao.
Kusaidia kupokea majalada,kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu
walipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI:-
Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au (VI) Sita aliyehudhuria
mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu, awe amefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe
amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na
serikali na kupata cheti.
NGAZI YA MSHAHARA: - TGS.B shilingi Laki tatu na elfu Tisini (390,000/=). kwa
Mwezi
4. MPOKEZI – NAFASI 1.
KAZI NA MAJUKUMU YAKE MPOKEZI:-
Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao
Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni
wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani
Kutunza na kudumisha usafi wa ‘’switchboard’’na ofisi yake
Kuhakikisha wageni wanaoingia ndani wana miadi au wamepata idhini ya
maafisa husika.
Kutunza Register ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na
zinazopigwa kwenda nje.
Kupokea simu toka ‘’Extension’’ za ndani na kupiga nje ya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) aliyefaulu masomo ya
Kiswahili, Kiingereza na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi simu
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
NGAZI YA MSHAHARA TGS. A Shilingi laki tatu na elfu kumi (310,000/=) kwa
mwezi
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:-
Maombi yote yaandikwe kwa mkono, na yaambatanishwe na vyeti pamoja na
nakala ya maelekezo binafsi (CV) ambayo imechapwa kwa mashine au kompyuta
na kusainiwa na mwombaji.
Maombi yatumwe kwa:-
MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA
S.L.P.1333,
MWANZA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28/08/2017 saa Tisa na nusu alasiri (9.30).
Hakuna maoni: