Ronaldo ametangazwa kuwa mchezaji bora UEFA 2016/2017


Baada ya Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo Alhamisi ya August 24 2017 mjini Monaco Ufaransa kuchezesha droo ya hatua ya makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, walitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017.
Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea Real MadridCristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017 kwa kumshinda mpinzani wake mkubwaLionel Messi wa FC Barcelona na golikipa wa Juventus Buffon.

Kutoka kushoto ni Messi, Buffon na Ronaldo
Ronaldo kwa msimu wa 2016/2017 ambapo ameshinda pia tuzo ya mshambuliaji bora 2016/2017, alikuwa na msaada mkubwa kwa club yake ya Real Madrid msimu uliyomalizika lakini ameifungia magoli 12 na kutoa assist 6 katika michuano ya UEFA Champions League.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.