Zilipendwa yaishusha Seduce Me katika trending

Vita ya trending katika mtandao wa YouTube haimuachi mtu salama!

Kwa mujibu wa mtandao wa YouTube unaotumika kuwekwa video mbalimbali za muziki, umeonyesha kuwa ngoma ya ‘Zilipendwa’ ya WCB imeshika namba moja katika trending huku ikifuatiwa na ‘Seduce Me’ ya Alikiba.
Hata hivyo ngoma ya ‘Seduce Me’ itabaki kuwa katika historia ya kuwa ngoma pekee Afrika Mahariki kuwa na views milioni mbili kwa wa siku tatu. Pia ngoma ya ‘Seduce Me’ itabaki katika historia ya kupiku ngoma ya ‘ Salome ‘ iliyofanywa na Diamond Platnumz na Rayvanny ambayo ilitazamwa na watu milioni 1 kwa siku mbili .

Ngoma hizo mbili zinafuatiwa na  Jux -Utaniua, Aslay – Pusha na Rostam (Roma & Stamina) – Hivi ama vile.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.