Mayweather awachana wanaompinga Trump ‘hamtaki kuambiwa ukweli
Mwanamasumbwi maarufu duniani, Floyd Mayweather Jr ameonekana kukerwa na baadhi ya wamarekani wanaomkosoa Rais wa Marekani Donald Trump kwa kuwambia kuwa wafanye kazi za maendeleo zitakazowaletea maendeleo na sio kulaumu kila siku.
Mshindi huyo wa Dunia wa ngumi za uzito wa juu amesema watu wengi nchini Marekani hawataki kuambiwa ukweli na ndiyo maana wanamchukia Trump huku akidai wanaoandamana wanapoteza muda tu badala ya kukaa nyumbani kupanga miradi ya biashara.
“Watu hawataki kuambiwa ukweli, unajua mwanaume lazima aongee kwa kumaanisha kama anavyofanya yeye ni mwanaume wa kweli, wanaume tunasema ‘yule mwanamke ni mzuri na wewe unaitikia ndiyo, kwa sababu unamuona, na lazima nimtafute nimpate’, najua unanielewa ninachomaanisha ?,”ameongea Mayweather kwenye kipindi cha Hollywood Unlocked kwa kuhoji.
Mayweather ameendelea kusema watu wasimchukie Rais Trump kwa vile yupo madarakani kwani kuongoza Marekani hakuteuliwa na mtu wala hakuiba kura bali ni wamarekani wenyewe walimchagua.
“Kipindi cha Nyuma wakati Trump mtu wa kawaida nilikuwa namuona kwenye WWE (Michezo ya mieleka) na kwenye show mbalimbali sikuwahi kusikia kuwa ni mbaguzi wa rangi lakini kwanini alivyoingia tuu madarakani haya mambo yakaanza kukua?, Naona hadi aibu kuwambia ukweli wamarekani wenzangu, huyu mtu (Trump) hajafanya chochote kile, kama hamkutaka aingie White House msingempa kura zenu, kwani inavyoonekana kama aliiba kura zenu, kumbe alitimiza majukumu yake na akachanguliwa na sisi wenyewe kwa kura zetu, “amesema Mayweather Jr.
Kuhusu sera za uhamiaji za Rais Trump, Mayweather pia ametia neno kwa kusema ni muda muafaka kwa Wamarekani kuwa wazalendo wa nchi yao kwani kumekuwa na wageni wengi wakiingia kila siku na kutengeneza fedha nyingi huku wazawa wakilalamika maisha magumu.
“Nakutana na watu wengi sana kutoka nchi mbalimbali hapa Marekani na nikiwauliza kwanini upo hapa? . wanasema ‘wanapapenda hapa, wanapenda na nchi zao pia’, sasa mimi nawauliza kama mnapenda nchi zenu kwanini mpo hapa? hujui kuwa unachukua nafasi ya wenzako?” amesema Mayweather huku akishangaa
“Kuna baadhi yetu hata kama kazi walizotangaza kuna Wamarekani wanajua kufanya, lakini utashangaa wanaajiriwa watu kutoka nje ambao hawajui kodi tunazolipa na ugumu tunaopitia, sijui nchi yetu ina watu wangapi wanaoishi kinyume na sheria hata nashindwa kukadiria.”amesema Mayweather huku akimkingia kifua Rais Trump juu ya sera yake ya kujenga ukuta kutenganisha Marekani na Canada.
“Ninachomaanisha hapa sio kumuunga mkono Trump kwenye sera yake ya kujenga ukuta na ile ya kuzuia safari kwa baadhi ya nchi hapana mimi nampenda kila mtu, nachekana watu wote kutoka kila nchi, ninaachomaanisha ni kwamba Floyd siogopi biashara ya mtu mwingine, watu wengi wanajikuta wanaogopa biashara za watu wengine, badala ya kujiangalia hao wenyewe vitu gani vinavyowaangusha wasifikie malengo, Mimi nimepambana mpaka kufikia hapa si kuwa na hofu ya nani anafanya nini? kwa sababu niliamini mimi ni Floyd,“amesema Floyd Mayweather kwenye mahojiano yake na kipindi cha Hollywood Unlocked.
Tazama mahojiano yake yote kwenye kipindi cha Hollywood Unlocked hapa chini.
Hakuna maoni: