Wabunge wa Upinzani Wagoma Kuingia Bungeni
Taarifa kutokea Bungeni Dodoma ni kuhusu Wabunge wa Upinzani wamegoma kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge wakati Mkutano wa Nane wa Bunge la 11 ukiendelea kwa madai kuwa hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa Wabunge 8 wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi CUF.
Mkutano wa Nane wa Bunge la Jamhuri umeanza leo Mjini Dodoma na moja ya mambo yaliyopo kwente ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa Wabunge wapya 8 wa Viti Maalumu ambao wameteuliwa kuziba nafasi za Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa CUF.
Hakuna maoni: