SINTOFAHAMU JUU YA KUPANDA KWA DIRECT COST UDOM. WATOTO WA MASIKINI NJIA PANDA
(UDOM) |
ANAANDIKA MDAU WA ELIMU UDOM
Mm kama mdau wa maendeleo kwa kizazi kilichopo na kijacho nahoji juu ya mambo yafuatayo kwa serkali ya wanafunzi udom maarufu kama UDOSO pamoja na uongozi wa juu wa chuo kikuu DODOMA (UDOM)
Tarh 19/09/2017 liliwekwa tangazo la kupanda kwa direct cost katka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM ) kama ifuatavyo.
Direct cost kupanda kutoka Tsh 169,000/= hadi Tsh 263,500/=
UDOSO FEES kupanda kutoka Tsh 5000/= hadi Tsh 10000/=
Lakin baada tu ya muda mfupi tunaambiwa Rais wa federation na makamo wake wamefanya mazungumzo na management ya chuo na kuja na majibu yafuatayo
DIRECT COST IWE TSH 750/= @siku ambayo ni sawa na Tsh 228,500/=
UDOSO FEES kuwa Tsh 5000/= kwa continuous, na first Year kuwa Tsh 10,000/=
maswali ya kujiuliza kwanini gharama ziongezeke UDOM tu?
je ruzuku imepunguzwa UDOM tu?
kwanini wanafunzi hawakushirikshwa kwenye kikao cha kuongeza hizo gharama?
Swali la pili kwa nn hili swala marais ,wazir wakuu na mawazr wa makazi wa college zote za udom msikutane kwa kikao cha dharula mkiwa na rais wa federation mkajadiri kwa kina na mkahoji sababu za msingi kwa nn Direct cost ipande kwa kiasi kikubwa hivyo ukizingatia Udom ni chuo cha serikali tena makao makuu ya nchi, lakin badala yake mmewaachia watu wa 2 tu ndio wakafanya maamuzi ya watu takiriban elf 30, kitu ambacho si busara hata kidogo,
Kwa ujumla ni kwamba hiyo taarfa ya federation ya kupunguza direct cost had 228,500/= bado tu itaathiri maisha ya wanachuo wengi sana hasa watoto wa kutokea familia maskini .
NB. Kwa ile direct cost ya 169000/= wanachuo wangapi walishindwa kufanya registration kwa wakat je hii mlio suggest hapo si ndio watu weng watapospond kabisa masomo,
Please Udoso katka kipindi hiki kigumu ni wakati mwafaka kwenu kutafakar juu hiyo direct cost .
wadau wa elimu na serikali mtusaidie katika hili lasivyo watoto wamasikini kusoma kwao itakuwa ni ndoto
YATAMBUE MABADILIKO DIRECT COST UDOM UDOM MWAKA WA MASOMO 2017/18. WATOTO WA MASKINI KUSOMA UDOM ITAKUWA NDOTO TU
Hakuna maoni: