Asensio ainusuru Madrid mbele ya Valencia
Klabu ya Real Madri ya Hispania hapo jana imetoka sare ya magoli 2-2 mbele ya Valencia huku ikikosa huduma ya mchezaji wake raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye anatumikia adhabu baada ya kumsukuma muamuzi katika mchezo wao uliyopita wakati kijana Marco Asensio akiibuka shujaa katika mchezo huo baada ya kuifungia timu hiyo mabao yote mawili.
Asensio mwenye umri wa miaka 21 alifungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao lake la kwanza akiwa umbali wa hatua 20 kutoka lango la Valencia huku mchezaji, Carlos Soler akiisawazishia na kisha Geoffrey Kondogbia akiifungia Valencia bao la pili.
Kijana wa Madrid, Asensio akaisawazishia timu yake na kupelekea kumalizika kwa sare hiyo ya 2-2. Katika mchezo huo mchezaji, Karim Benzema alipoteza nafasi nyingi za wazi.
Kwa matokeo hayo inaifanya klabu za Real Sociedad, Barcelona na Leganes zinaongoza msimamo wa ligi hiyo ya Hispania La Liga kwakuwa na alama sita huku Atletico Madrid, Levante na Real Madrid zikishika nafasi ya pili kwa alama nne .ambao walikuwa bila mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo aliyepigwa marufuku, walimchezesha kiungo wa kati Casemiro safu ya ulinzi kwani Sergio Ramos bado anatumikia marufuku.
Hakuna maoni: