Bosi wa kampuni ya Samsung afungwa jela miaka 5.


Mahakama ya Korea Kusini imemuhukumu bosi wa kampuni ya Samsung, Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la utoaji rushwa.
Bilionea huyo ambaye pia ni makamu wa rais wa kampuni hiyo ya utengenezaji vifaa vya umeme alishtakiwa kwa kosa hilo ambalo pia lilisababisha aliyekuwa rais wa nchi ya Korea Kusini, Pak Geun-hye kuondolewa madarakani.
Mbali na kosa hilo la utoaji rushwa ambalo alishtakiwa nalo, makosa mengine yaliyokuwa yanamkabili ni pamoja na wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi.
Hata hivyo wakili wa tajiri huyo, Song Wu-cheol amedai kuwa anaamini mahakama itabatiisha hukumu hiyo. Lee Jae-yong alikalia kiti cha uongozi katika kampuni ya Samsung kuanzia mwaka 2014 baada ya baba yake kupatwa na aradhi ya mshtuko wa moyo
.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.