Filamu ya San Andreas yasaidia kuokoa maisha ya mtoto


Filamu ya San Andreas, iliyoigizwa na nyota wa filamu Dwayne Johnson, maarufu kama The Rock amemtaja mvulana wa miaka 10, kuwa ni shujaa baada ya kufanikiwa kuokoa maisha ya nduguye.

Jacob O’Connor akiwa na mdogo wake Dylan
Kijana huyo aitwaye Jacob O’Connor alimuokoa ndugu yake Dylan(2) aliyekuwa katika ndibwi la maji, hivyo Jacob alitumia mafunzo aliyopata kupitia filamu hiyo kuokoa maisha ya mdogo wake.
Baada ya kumuokoa mdogo wake alimpatia huduma ya kwanza kwa kumpatia hewa kama alivyofanya The Rock, baada ya kumuokoa binti yake katika filamu hiyo.
Dylan alikimbizwa hospitali kwa matibabu na aliweza kupata nafuu. Filamu ya San Andreas ilitoka mwaka 2015.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.