Dayna Nyange aungana na A.Y, Diamond na Vanessa Mdee katika hili
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amezungumzia muonekano wake mpya baada ya kuweka meno ya gold.
Wasanii kadhaa wa Bongo Flava wameshafanya hivyo miongoni mwao ni AY, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Dogo Janja lakini katika mtindo wa kuweka na kutoa.
Muimbaji huyo amesema wasanii wengi walifanya hivyo lakini walikuwa wananunua yale meno ya kuweka na kutoa lakini alivyoweka yeye ni tofauti kwani huwezi kuyatoa hadi pale atakapoenda kwa wahusika ili kuyatoa.
“Niliwekea South Africa, unaweka booking for four days or one week, wanaenda wanakuchonga meno kidogo then wanaweka, kwa hiyo siyo kitu ambacho naweza kusema sasa hivi nataka kukituoa nikaweza,” Dayna ameiambia Bongo5.
“Sijajua kwa Wabongo kama naweza nikapata hiyo huduma kwa sababu nilishawahi kujaribu kuweka kikaja kikatoka wakati nafanya video ya Komela, kwa kuwa hakikua na utaalam,” ameongeza.
Dayna ameendelea kwa kusema alipoenda ku-shoot video yake mpya ‘Chovya’ South Africa ndipo alipotumia fursa hiyo kufanya hivyo kwa mara ngingine tena.
“Nikaona let do it, so nikawa nimeweka, ni gold huwezi kuweka bati mdomoni unaweza kuharibu utumbo. Thamani yake si kubwa sana, dola kadhaa tu,” amesema Dayna.
Hakuna maoni: