FLOYD MAYWEATHER HANA KINYONGO NA UTABIRI WA JUSTIN BIEBER


Ikiwa zimepita siku chache tangu msanii wa Pop Justin Bieber atabiri kuwa bondia Conor McGregor, atashinda mpambano unaotarajiwa kufanyika leo hu na kuacha kumtaja swahiba wake Floyd Mayweather kuibuka na ushindi, hatimaye Floyd ameamua kunena ya kwake kuhusu utabiri huo.
Akipiga stori na ‘Hollywood Unlocked’ Floyd ameeelea video ya Justin aliokuwa akihojiwa na TMZ ambapo alitabiri kuwa Conor McGregor ataibuka na ushindi na sio Flody, ndipo bondia huyo wa TMT asema kuwa hana tatizo na msanii huyo wa pop na kila mtu anamaono yake hivyo hawezi kuingilia anachokifanya mtu.
Mpambano wa Floyd Mayweather na Conor McGregor unatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa T-Mobile Arena jijini Las Vegas- Marekani.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.