Hizi hapa video 5 za Bongo Flava ‘zinazotrend’, vita ni Alikiba na Diamond
Katika chart ya wiki hii kuna mabadiliko makubwa kwani katika video tano za wiki iliyopita zimebaki mbili tu ambazo ni Rostam (Roma & Stamina) – Hivi Ama Vile na Lava Lava – Dede.
- Alikiba – Seduce Me (pia katika trending ya Tanzania ni namba moja) wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Rostam (Roma & Stamina) – Hivi Ama Vile.
2. Diamond, Harmonize, Rich Mavoko, Rayvanny, Queen Darleen – Zilipendwa (katika trending ya Tanzania ni namba mbili) wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Lava Lava – Dede.
3. Jux – Utaniua (katika trending ya Tanzania ni namba nne), wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Rayvanny – Chuma Ulete.
4. Rostam (Roma & Stamina) – Hivi Ama Vile (katika trending ya Tanzania ni namba 16), wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Aslay – Baby.
5. Lava Lava – Dede, wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Gigy Money – Papa.
Hakuna maoni: