Ndege yamsafirisha kiungo wa Azam FC kufanyiwa vipimo

Mchezaji wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Joseph Kimwaga amerejea Dar se salaam hapo jana kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa goti lake la mguu wa kushoto lililopata mshtuko.
Kimwaga aliyekuwa ameanza kurejea vema kwenye kiwango chake kilichomtambulisha huko nyuma, amepata majeraha hayo kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu cha TTC cha mkoani Mtwara, Alhamisi iliyopita wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda.
Mshituko wa goti lake umekuja ghafla wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Ndanda alipokuwa akihitaji kupiga mpira na kujikuta akishindwa kukanyagia mguu
Baada ya tukio hilo, Kimwaga alipatiwa huduma ya kwanza na daktari wa timu, Mwanandi Mwankemwa, kabla ya kukimbizwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara kupatiwa matibabu ya awali na kusahauri apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ili kufanyiwa kipimo cha MRI kubaini undani wa tatizo lake.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Idd, amesema kuwa mchezaji huyo tayari amewasili jijini hapa tayari kabisa kufanyiwa kipimo hicho kesho Jumatatu.
Idd amesema kuwa mara baada ya kufanyiwa kipimo hicho, itajulikana kama tatizo alilonalo litaweza kutibiwa nchini au kusafarishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi ili kuokoa kipaji chake.
Hii ni mara ya pili Kimwaga kuumia kwenye goti lake hilo, mara ya kwanza alivunjika miaka mitatu iliyopita hali iliyofanya kupelekwa nchini Afrika Kusini kufanyiwa matibabu na kurejea tena uwanjani.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.