Mafuriko sio Dar tu, yamewakuta ndugu zetu wa Houston, Marekani (+Picha 20)
Zaidi ya watu 2,000 wameokolewa baada ya mafuriko katika Mji wa Houston huku Kimbunga Harvey kikiendelea kusababisha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Texas, Marekani huku kukiripotiwa pia vifo kadhaa na uharibifu mkubwa kutokana na nguvu za maji.
Gavana wa Texas Greg Abbott amewaambia Wanahabari kuwa hawezi kuthibitisha vifo vinavyodaiwa kutokana na mafuriko hayo huku Meya wa Houston Sylvester Turner akisema hadi kufikia Jumapili jioni, Polisi wa Houston na Idara ya Zimamoto walipokea simu za kuomba msaada zipatazo 6,000 na waokozi wameokoa zaidi ya watu 1,000.
Hakuna maoni: