MANGE ANANIPENDA NA ANANIKUBALI- WOLPER
Msanii filamu Bongo, Jacqueline Wolper amedai kwa sasa hana beef na Mange Kimambi kwani ni mtu ambaye anampenda na kumkubali.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/08/20905567_459896187759416_23984394460987392_n.jpg)
Wolper na Mange walikuwa katika mgomvi wa kurushia maneno makali katika mitandao ya kijamii siku za nyuma.
Muigizaji huyu ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa hana ugomvi wowote na kabla ya ugomvi wao walikuwa wanaelewana vizuri ila Mange alifikia hatua hiyo kutokana na hasira.
“Kitu kimoja ambacho watu hawaelewi sina beef na Mange labda wanaona hivyo mambo ya mitandao na nini, halafu Mange hakuwahi kunichukia. Mimi Mange ameanza kunichukia baada ya kuanza kumpost mheshimwa lakini siku zote hakuwahi kunichukia na ananipenda na ananikubali,” amesema na kuongeza.
“I know that na mimi pia nampenda ndio why namfollow nalike picha zake. Kwa hiyo mimi naona ni mtu kafanya vitu kwa hasira na sidhani kama amefanya kutoka moyoni mwake au amefanya kwa chuki,” amesisitiza.
Hakuna maoni: