Nje ya muziki, fahamu kazi nyingine ya Lamar
roducer kutoka studio za Fish Crab Lamar amewaka wazi kazi ngingine ambazo anafanya kwa sasa.
Lamar ameiambia XXL ya Clouds Fm kwa sasa anafanya biashara ya kuuza vifaa vya magari na kusimamia Car Wash yake ingawa bado anafanya muziki na kazi zote anazifanya kila siku.
“Mimi kila kitu ni biashara, muziki ni biashara kwa sababu bila muziki nisingefika hapa, muziki umenipatia umaarufu ambao umenipatia uaminifu kwa watu” amesema.
“Hata Jaffarai ananisapoti kwa sababu yeye yupo katika biashara hii kwa muda mrefu, halafu sio kwamba nimemuingilia kwenye biashara yake kwa sababu hata studio zipo nyingi, arts siku hizi wanamilikia studio, Diamond anamiliki studio,” ameongeza.
Hakuna maoni: