RC Makonda awataka watumishi kupenda kazi kuliko mshahara
Wauguzi na madaktari wametakiwa kuwa wavumilivu wanapotoa huduma kwa wagonjwa licha ya changamoto ambazo wanazo zipata wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alipokwenda kutembelea hospitali mpya ya mama na mtoto iliyopo Chanika wilayani ilala jijini humo.
“wapo wakina mama ambao watakao kuja wakiwa na hasira na kukujibu majibu yasiyo mazuri , wengine utakuta wanakusonya tu bila sababu yeyote ,mwengine anweza hata kukutemea mate, basi chukulia ni moja ya sehemu yako ya kazi wala usijibizane nae”Alisema Paul Makonda.
Makonda amewataka madaktari na wauguzi hao kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kuwahudumia wote bila ya kujali rangi,sura,wala kabila na hata uwezo wa kipato chake.
“Hakikisheni mnatoa huduma nzuri ili wakawe mabalozi wazuri huko kwenye makazi yao, na wakaitangaze hospitali ya chanika kuwa ni yenye kutoa huduma nzuri”Älisema Makonda.
Makonda amebaini upungufu wa madaktari ambapo amewaomba kufanya kazi kwa jitihada ili kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri.
Makonda amebaini upungufu wa madaktari ambapo amewaomba kufanya kazi kwa jitihada ili kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri.
“Tunajua kama tunaupungufu wa Madaktari na wauguzi katika vituo vyetu vingi vya mkoa wetu wa Dar es salaam kwa mantiki hiyo tutalazimika kufanya kazi ngumu kidogo, kwa sababu nafasi ya mtu mmoja inapaswa kuchukua nafasi ya watu wawili au watatu, kwa wewe uliopo hapa unatakiwa kufanya kazi kama watu watatu”Alisema Paul Makonda.
Hospitali hiyo imengwa na wadau wa maendeleo kutoka Korea kusini, ambapo hospitali hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na hivi karibuni itaanza kutoa huduma kwa mama na mtoto.
Hakuna maoni: