Mastaa waungana kuiombea Huston baada ya kukumbwa na mafuriko
Mastaa kadha kutoka Marekani, wameamua kuungana na kutaka kuchangia waathirika wa mafuriko yaliyoikumba jimbo la Huston Marekani.
Mafuriko hayo yamesababishwa na kimbunga cha Harvey, kijichotokea katika jimbo hilo na katika maeneo mengine ya mji. Mpaka sasa imeripotiwa kuwa watu 2,000 wameokolewa kutoka na kimbunga hicho na wawili wamesadikika kufa maji.
Mastaa kama Kervin Hart, 50 Cent, Nick Minaj wameamua kuunga mkono kampeni iliyoanzishwa ya kuombea mji huo na kutoa msaada kwa waathirika wa tukio hilo.
Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa (NWS) imesema hali ambayo inashuhudiwa katika maeneo mbalimbali katika jimbo hilo haijawahi kutokea, pia idara hiyo imesema kuwa mafuriko yaliyotokea katikati mwa mji huo bado wanendelea na uchunguzi.
Hakuna maoni: