Vita ya ‘trending’ YouTube imebaki kwa Seduce Me na Zilipendwa
Wimbo mpya wa Alikiba ‘Seduce Me’ ulioachiwa Ijumaa hii unaendelea kutrend kupitia mtandao wa video wa YouTube huku nafasi ya pili ukifuatiwa na wimbo mpya wa WCB, Zilipendwa.
Video ya muimbaji huyo wa RockStar400 mpaka sasa ina views 540,320 ikiwa ni video ya kwanza kuachiwa kabla ya WCB iliyoachiwa jioni yake.
Video ya WCB ‘Zilipendwa’ mpaka sasa ina views 222,962 ikiwa ina saa 12 toka iachiwe kupitia YouTube.
Kitendo cha WCB kuachia video ya wimbo huo muda mchache baada ya Alikiba kuachia Seduce Me, kumewafanya mashabiki wa wasanii hao kushindanisha project hizo mbili ambazo bado zinashindana kupitia mtandao wa YouTube.
Wawili hao kila mmoja anaonyesha bado ana hasira na mwenzake kwani kila mmoja anamtishia mwenzake ataachia ngoma nyingine.
Alikiba anadaiwa kutweet kwamba wimbo ‘Secude Me’ alikuwa anatesh mitando huku akidai ngoma kamili inakuja.
Kwa upande wa Diamond naye kupitia meneja wake Sallam amedai kwamba baada ya ‘Zilipendwa’ wataachia wimbo mpya ambao Diamond ameshirikiana na msanii mkubwa wa kimataifa.
Hakuna maoni: