JINSI YA KUPANGA BEI NAKUPATA FAIDA KWENYE BIASHARA YAKO..!!! SOMA HAPA


Images



Jijengee mazingira ya kupata faida endelevu. Ikiwa unafanya aidha biashara ya huduma au bidhaa, ni muhimu kutathmini bei ya bidhaa uliyopanga ili kupata faida endelevu. Jiulize je bei uliyopanga inaendana na uhalisia katika soko?

Hili la upangaji wa bei za bidhaa ni jambo la msingi kulifikiria kwani ni hapa ambapo tunaweza kujenga faida endelevu. Usifikiri kupanga bei ya chini ndio njia ya kuvutia wateja au kupanga bei ya juu ni kufukuza wateja, la muhimu ni kucheza na soko.

Mara nyingi katika upangaji wa bei za bidhaa kuna vitu vingi vya kuangalia, kwa mfano upatikanaji wa bidhaa ukiwa mwingi hushusha bei za bidhaa husika, na hali kadhalika upatikanaji wa bidhaa ukiwa adimu bei za bidhaa husika huwa juu.

Sasa mjasiriamali ili kujenga mazingira mazuri ya kupata mafanikio, ni muhimu kuwa na uwezo wa kucheza na soko lako. Mara nyingi nafurahishwa jinsi ‘wamachinga’ wanavyopanga bei za bidhaa zao wanapokuwa katika mihangaiko yao ya kila siku.

Kwa kawaida bei anayoanzia nayo katika moja ya bidhaa zake na bei ambayo mwisho wa siku mtakubaliana naye huwa tofauti. Kwakuwa wao wanajua gharama za bidhaa husika, huwa hawachezi mbali ili kuweza kufidia gharama hizo na kupata faida kidogo.

Vivyo hivyo kwa wajasiriamali wengine hawana budi kuacha kujifunga tu na bei moja badala yake hawana budi kucheza na soko. Zipo bidhaa ambazo bei zake hazina majadiliano, lakini pia kuna bidhaa ambazo mazungumzo yanaweza kuwepo.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.