JIFUNZE KUWA NA SOKO LAKO KUTOKANA NA BIASHARA UNAYOFANYA..!!!!! SOMA HAPA


Jitengenezee soko lako maalum. Kama ungependa biashara yako ifahamike kati ya biashara nyingine ni muhimu kuwa na soko lako maalum linaloeleweka. Hii ni njia ya pekee ya kukutofautisha na washindani wako.
Ni jambo la kupendeza kwa mfano mwanasheria fulani akafahamika kama mjuzi katika eneo fulani la fani yake kama vile madini, bima, kodi nakadhalika ili kuweza kujenga soko lake. Vivyo hivyo kwa wajasiriamali wanapaswa kutengeneza masoko yao maalum.

Kwa wale wenye kufanya biashara ya nguo aidha mitumba au nguo mpya, ni muhimu kutengeneza soko maalum la kile unachofanya. Yafaa watu wakufahamu kama mfanyabishara wa nguo fulani mwenye kulenga watu fulani kama wateja wako.

Ndugu mjasiriamali yafaa kukumbuka kuwa kuna fursa nyingi sana za biashara ambazo watu wanaweza kuzitumia, tatizo lililopo ni lile la watu kufanya mambo kimazoea. Lakini kama watu wangefanyia kazi fursa hizi ingetoa nafasi kwa wao kupata mafanikio.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.