KUFANYA TATHMINI YA MAFANIKIO ULIYOPATA INASAIDIA KUJUA WAPI UMESHINDWA..!!! SOMA HAPA


Jipime umefanya nini kujenga mafanikio. Baada ya mihangaiko ya hapa na pale, kule na huko wakati mwingine kushindwa hata kulala au kuhatarisha maisha yako katika safari mbalimbali, jiulize je, umefanikiwa kupata kile ulichotaka?

Lazima ifike mahali ujifanyie tathmini ya kile amabacho umefanya kwa siku, juma mwezi au mwaka, epuka kufanya mambo kimazoea kwa kuwa tu unapata hela ya kula na kukidhi mahitaji yako mengine, ni muhimu kwa wajasiriamali kujipima wenyewe. 

Tunapozungumzia kupima mafanikio katika biashara yafaa kutofautisha na ile hali ya wewe kukidhi mahitaji yako ya msingi kama vile chakula, mavazi, malazi na matibabu. Kaa chini uangalie nini umepata na kwa kiasi gani na kama ilipasa ufike hapo au zaidi. 

Lakini kwa mjasiriamali kupima mafanikio ni kuangalia mtiririko mzima wa kile ulichofanya kwa kipindi fulani. Unapojifanyia tathmini ya mafanikio yako pia ni moja ya njia ya kuweza kuangalia pale ambapo ulishindwa, na kujua nini kifanyike.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.