KUBISHANA KWENYE MAHUSIANO NI KUBORESHA MAPENZI YENU..!!! SOMA HAPA




kubishana sio ukorofi inategemea mnabishanaje na kuhusu nini? Katika hali halisi kubishana kwenye uhusiano kunahashiria afya ya uhusiano wenu....ikiwa kuna watu wanaishi pamoja kama wapenzi na hawajawahi kubishana basi ni either wanadanganya au mmoja wao anamuogopa mwenzie.

Pamoja na kuwa ninyi ni wapenzi bado mnatofautiana kijinsia, kimawazo, kikazi, kipato, matumzi binafsi ya pesa, kimalezi na hata kasoro zenu hazifanani....hivyo kubishana ni lazima ikiwa kunatofauti hizo na nyingine ambazo unazijua.

Kubishana kunaweza kuwasaidia mmoja wenu kujirekebisha kwani itawawezesha
kutambua kosa lako ni lipi hasa kama mwenza wako sio mtu wa kukosoa papo kwa hapo (kosa linapotokea),


 Pia itakuwa nafasi nzuri ya kutambua au kugundua nini hasa mwenzako anafikiria kuhusu kosa/tendo ulilofanya au tabia yako na nini anataka kifanyike ili kuepuka mabishano ya mara kwa mara.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.