Natamani sana kufanya kazi na Alikiba – Bill Nass
Msanii wa Bongo Flava, Bill Nass ameeleza kuwa moja ya mipango yale ni kufanya kazi na Alikiba kwa siku za mbeleni.
Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sina Jambo’, ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa anatamani kufanya hivyo ila ni kitu ambacho anatakiwa kujipanga zaidi.
“Natamani sana kufanya naye kazi lakini unapofanya kazi na mtu kama Ali iwe kazi kubwa kulingana na ukubwa wake na game inavyoenda. Staki tu nitoke huku chini nifanye naye wimbo kwa sababu yeye tayari ameshamaliza, kwa mfano nikifanya naye wimbo usipofika popote itaniathiri mimi,” amesema Bill Nass.
“Kwa hiyo natamani kufanya naye kazi lakini iwe kama ambavyo Watanzania wanaweza kutarajia, nataka wimbo ambao naona huu unamfaa mtu kama Alikiba,” ameongeza.
Bill Nass amesharikiana na wasanii kadhaa wanaoimba katika ngoma zake akiwemo TID, Nazizi kutoka nchini Kenya na Barnaba.
Hakuna maoni: