Habari Njema: Wakazi wa Dar kupimwa afya bure! (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anawatangazia wananchi wote wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni ya Upimaji wa Afya Bure kuanzia siku ya Jumatano ya Septembe 06 -10 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

RC Makonda akiwa na madaktari ambao wataendesha shughuli hiyo.
Zoezi hilo litaendeshwa na Madaktari bingwa na Wauguzi zaidi ya 200 kutoka Hospital za Umma, Jeshi na za Watu Binafsi zilizomuunga mkono RC Makonda.
Makonda amesema kuwa hatopenda kuona Mwananchi anapoteza maisha kwa kukosa huduma ya Afya ndio maana ameamua kuendesha zoezi la upimaji wa Afya Bure ili Wananchi wapate fursa ya kujua Afya zao na kuwa na utaratibu wa kupima Afya zao mara kwa mara.
Aidha amezipongeza Hospital na zilizomuumga mkono ikiwemo Muhimbili, Ocean Road, Amana, Temeke, Mwananyamala, Muhimbili, TMJ, Sanitas, Agha Khan, Regency, Kairuki, TANCDA, IMMI Life, APHTA, CCP Medicine, MDA, NHIF, Wandile wa kaya, P Consult, Besta Diagnestics, Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Jamii Bora na Damu salama.
Makonda amesema watakaopimwa na kubainika kuwa na matatizo ya kiafya watapelekwa Hospital na kupatiwa matibabu Bure.
Hata hivyo amesema kuwa kutakuwepo na vifaa tiba vya kisasa, Magari ya kubeba Wagonjwa, Vyoo, Sehemu za watoa huduma na Sehemu za kupumzika wakati wa kusubiri huduma.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.