HISTORIA KWENYE TECHNOLOJIA YA KOMPYUTA.
1. PROCESSOR YA INTEL
“Processor” ni sehemu kwenye kompyuta ambayo inahusika na ukokotozi, uendeshaji na uchakataji wa kila jambo linaloendelea katika kompyuta. Kwa kifupi humithilishwa/hufananishwa na ubongo wa wanadamu.
Na “Processor” ndiye boss mkubwa sana wa Vibarua kwenye Kompyuta, na akilemewa kwenye Kompyuta anazimia, na kwa sababu yeye ndiye boss na akishindwa Kompyuta huzima ghafla.
Vibarua anaofanya nao kazi wamekubali kufanya kazi kwa pamoja kila mmoja akitekeleza kwa wakati. Vibarua hao ni kama RAM, Hard Disk na “Chip/Component” na Umeme, ambapo hizo “chip” zimeunganiswa kiprogram kuendesha mfumo mzima wa kikazi kwenye Kompyuta.
Leo hii tunapenda kueleza kwa ufupi kuhusu historia ya “Processor” ijulikanayo kama INTEL,
Kampuni hii ya INTEL ilianzishwa na Julai 18, 1968 na wanasayansi Robert Noyce pamoja na Gordon Moore, baada ya hapo walianza mchakato wa kutengeneza Proceesor hii ya Intel yakiwa ni maono waliyokuwa nayo.
Kwa mara ya Kwanza mwaka 1971 Walitengeneza “Processor” ya kwanza iliyojulikana kwa jina la “INTEL 4004(1971) Ikiwa na uwezo wa ufanyaji kazi/spidi(Clockrate) 740khz.
Baada ya hapo mtiririko wa utengenezaji wa “Processor” uliendelea kama inavyooneshwa hapo chini.
Intel 8080 (1972) ikiwa na spidi ya 0.2 hadi 0.8mhz.
Intel 8080 (1974) ikiwa na spidi ya 2mhz.
Intel 8086 & 8088 (1978 & 1979) ikiwa na spidi ya 5 hadi 10 mhz.
Intel 80186(1982) ikiwa na spidi ya 6 hadi 25mhz.
Intel 80286(1985) ikiwa na spidi ya 6 hadi 25mhz.
Intel 80486(1989) ikiwa na spidi ya 16 hadi 150mhz.
Intel Pentium 80501(1993) ikiwa na spidi ya 60 hadi 66mhz
Intel Pentium Pro (1995) ikiwa na spidi ya 150 hadi 200mhz
Intel Pentium II (Klamath) (1997) ikiwa na spidi ya 233, 266, hadi 300mhz
Intel Pentium II (Deschutes) (1998) ikiwa na spidi ya 333mhz
Intel Pentium II (Dixon) (1999) ikiwa na spidi ya 400mhz
Intel Pentium 3 Katmai (1999) ikiwa na spidi ya 450mhz 600mhz
Intel Pentium 3 Coppermine (2000) ikiwa na spidi ya 500 hadi 1133mhz
Intel Pentium 3 Tualatin (2001) ikiwa na spidi ya 1000hadi 1400mhz
Intel Pentium 4 Willamette (2000) ikiwa na spidi ya 1300 hadi 2000mhz
Intel Pentium 4 Northwood (2002) ikiwa na spidi ya 1600 hadi 2800mhz
Intel Pentium 4 Prescott (2004) ikiwa na spidi ya 2400 hadi 3067mhz
Intel Pentium 4 Prescott 2M (2005) ikiwa na spidi ya 2.8 hadi 4Ghz
Intel Pentium 4 Cedar Mill (2006) ikiwa na spidi ya 3 hadi 3.6Ghz
Intel Pentium 4 Gallatin (2003) ikiwa na spidi ya 3.2 hadi 3.4Ghz
Baada ya kupitia kipindi chote hicho ndipo Kampuni ikaingia kwenye mfumo wa Dual Core ambapo zilitengenezwa aina mbalimbali za “Processor” za Intel.
Nazo ni kama ifuatavyo,
Intel Pentium Dual Core
Intel centrino 2
Intel Centrino 2V pro
Intel Atom
Intel core 2 Duo
Intel core 2 Quad
Intel core 2 Extreme
Intel VIIV.
Baada ya hapo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011 hadi 2017 Kampuni hii imekuwa na mabadiliko makubwa kwa kusababisha kuwa na “Processor” zenye uwezo mkubwa katika utendaji katika Kompyuta kwa ujumla.
Hapa tumeshuhudia teknolojia ya Processor ndani ya Intel ikiingia kwenye mfumo wa Core i3 hadi Core i9.
Kwenye upande wa Processor zote hizo za Core i3 hadi Core i7 zimekuwa zikipitia vipindi(generation) tofauti tofauti, hapa tunaona kuna kipindi cha kwanza hadi cha nane (1st generation hadi 8th generation), na uwezo/spidi ya Processor huanzia 2.ghz hadi 3.9ghz.
Ilikuwa tarehe 23/08/2017 siku ambayo Kampuni ya Intel walianzisha Processor ya Core i9.
Lengo la kueleza suala zima la Processor ni kukueleza ni “Processor” ipi utumie kutokana na maendeleo ya teknolojia lakini pia kutokana na matumizi ya Kompyuta kulingana na kazi zako.
Iko vizuri historia...
JibuFuta