MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KOMPYUTA..



 UTUMIAJI/MATUMIZI (USABILITY).
Ni kipindi hasa cha Wanafunzi wengi kuelekea Vyuoni na wengi wao watapenda kununua Kompyuta kwa ajili ya Masomo/Kozi mbalimbali  huko waendako
Kwa kutambua nafasi hii ya Kielimu juu ya Matumizi ya Kompyuta nasi tumeona ni vyema kutoa Elimu hii, ili angalau kuwa na uelewa zaidi maana tunatambua kuwa wapo wenye uelewa juu ya somo hili lakini pia wapo ambao bado hawana uelewa hivyo ni vyema tusome kwa umakini kabla ya kununua Kompyuta yako kwa matumizi uwapo masomoni.

Kabla ya kununua Kompyuta kwa ajili ya matumizi yako ni vyema kutambua unanunua kompyuta kwa ajili ya kazi gani, mfano kama unanunua Kompyuta kwa matumizi ya kawaida kama vile kutuma email,kutumia kwa ajili ya mitandao ya kijamii hata kuchapa kazi za kawaida waweza kutumia Kompyuta zenye uwezo wa kawaida tu, lakini Kama unafanya kazi za kuchora ramani, kufanya “video editing”ni vyema kutumia Kompyuta yenye uwezo mkubwa sana.
9. BEI (PRICE)
Pia ni vyema kuangalia bajeti yako mfukoni, usije ukanunua Kompyuta kwa bei kubwa ukashindwa hata jinsi ya kuendesha maisha yako ya kawaida.
8. MFUMO WA UTENDAJI WA KOMPYUTA YAKO (OPERATING SYSTEM TYPE).
Angalia pia mfumo wa utendaji wa Kompyuta, hapa tunaangalia “window” inayotumika kwenye Kompyuta yako, maana kuna baadhi ya window zimepitwa na wakati na haziwezi kukubalika kwa baadhi ya Program/Software kwenye Kompyuta yako Mfano, Window Vista Imepitwa na wakati halafu unanua Kompyuta yenye window hiyo.
7. MWONEKANO (SIZE)
Hapa wengine unakuta wanapenda Kompyuta yenye kioo/screen kubwa, wengine kioo/screen ndogo.
Kwa kawaida screen/kio huanzia inch 13 hadi 17.
6. KUUNGANIKA(PERIPHERALS)
Hapa tunaangalia kwa jinsi gani Kompyuta yako inaungana na vifaa vingine kama “Printer” na “scanner” pia angalia kama Kompyuta yako una uwezo wa kuweka CD,DVD n.k au kama kuna sehemu ya kuweka “flash disc”.
5. BRAND
Hapa inategemea na jinsi wewe unapendelea “Brand” ipi ambayo ungependa kutumia, zipo brand mbalimbali kama Dell, Sony, HP, sumsung, Acer, Asus, n.k sasa wewe hapo utakuwa umeishachagua brand ambayo ungependa kuitumia katika kazi zako.
4. UKUBWA WA NDANI WA KOMPYUTA YAKO (HARD DISK)
Hiki ni kitu muhimu sana ambacho yafaa ukazingatia hasa pale unapotaka kununua Kompyuta yako kwa mara ya kwanza, Mfano hapa utakuta upo ukubwa wa 80GB, 160GB,320GB,500GB,1TB sasa wewe ili uweze kununua ukubwa hapa utaangalia ni ukubwa upi wafaa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu zako kwa ujumla
3. RAM
Ram, hii husaidia katika kuongeza ya utendaji wakazi wa Kompyuta yako hasa pale unapokuwa unasoma au unachapa kazi zako, hii hufanya kazi pamoja na Hard Disc na kutoa taarifa haraka kwenye mfumo wa Kompyuta kwa ujumla.
Hivyo ni vyema sana kuangalia ukubwa wa Ram yako, mfano utakuta kuna DDR3 Ram, DDR2 hata ukubwa tofauti kama 2GB,4GB,8GB,16GB n.k.
2.PROCESSOR
Hii kwenye Kompyuta hufanya kazi kama “ubongo” kwenye mwili wa mwanadamu, kwa kawaida processor, hupokea habari, hubeba habari, hutafsiri na kutoa taarifa kwa vifaa vingine kwenye Kompyuta.
Hivyo pia kuwa makini sana pale unapotaka kununua Kompyuta yako, ukizingatia jinsi utumiaji/matumizi yako ya Kompyuta yatakavyokuwa, kwa mfano utakuta mtu ananunua Kompyuta yenye “Dual Core” huku anafanya kazi ngumu sana kama kuchora ramani, “video editing” hapa utakuta lazima utendaji utakuwa wa kusuasua.
Kwa kipindi hiki watu wanapenda Kompyuta zenye “Processor” yenye uwezo wa “Core i3, Core i5”, “Core i7” zenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa wepesi sanasana.
1.WARRANTY
Pia ni jambo jema sana kuangalia “warranty” ya kompuyta yako, hapa kama haijawekwa kwenye sticker itakubidi kumuuliza anayekuuzia kwa ajili ya ulinzi Zaidi wa kifaa chako pale kipatapo Shida yoyote.
 Image result for KUNUNUA  COMPUTER

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.