Kiongozi serikalini ampigia saluti Alikiba

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi ameweka hisia zake hadharani kwa kumsifia Alikiba kwa uzuri wa wimbo wake  mpya wa ,Seduce me’ huku  akiahidi kumpatia zawadi yoyote aipendayo.
Picha inayohusiana
Alikiba
Mhe. Hapi ameshindwa kuzuia hisia zake juu ya wimbo huo mpya wa Alikiba ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo aachie ngoma hiyo  baada ya kukaa mwaka 1 na miezi kadhaa tangu alipotoa wimbo wake wa Aje .
“Nimekuelewa sanaa wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule.Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli.Keep the fire burning!”,ameandika Mhe Ally Hapi.
Wimbo huo ambao tayari umeshavunja rekodi ya kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Tanzania unaonekana kuwazutia mastaa kibao hapa nchini akiwemo Wema Sepetu.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.