Mahakama nchini Kenya yapiga kalenda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi


Mahakama Kuu nchini Kenya imesogeza mbele muda wa kuanza kusikiliza Kesi ya kupinga ushindi wa Rais mteule wa Kenya,Uhuru Kenyata, iliyotakiwa kuanza kusikilizwa leo na badala yake itaanza kusikilizwa kesho.

Kiongozi wa kambi ya upinzani, Raila Odinga
Kesi hiyo iliyopangwa kuanza kusikilizwa leo jumatatu jioni baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza iliyofanyika jana kwa pande zote tatu yaani upande wa NASA, Jubilee na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) kuwasilisha mahakamani hoja zao za maandishi.“Ratiba ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo utaanza kesho kuanza saa tatu asubuhi,“ ni kauli ya Msajili wa Mahakama hiyo, Esther Nyaiyaki ambaye alinukuliwa na gazeti la Kiingereza la Standard nchini humo bila kueleza mabadiliko hayo yametokana na jambo gani.
Kesi hiyo inatokana na uamuzi wa Muungano wa vyama vya upinzani NASA chini ya mgombea wake Raila Odinga kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, wakidai kuwa haukuwa wa haki na huru.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.