Siri ya Bill Nass kutoa ‘hit songs’
Msanii wa Bongo Flava, Bill Nass amesema kuendelea kujifunza vitu vipya katika muziki ndio sababu ya kuendelea hit song.
“Kikubwa ni kuendelea kukomaa, kuendelea na kasi kwa sababu muziki kila siku unakua, kwa hiyo kama mimi sikuwi nipo pale pale ina maana muziki utamuacha,” ameiambia Bongo5.
“Kwa hiyo ni kuendana na kasi ya muziki namna unavyokua , pia kuna vitu vipya nimevipanga na tumeanza na Sina Jambo, tumewekeza humo tunataka tuone ni namna gani tunaweza tukapata faida tukawekeza katika project nyingine all in all ni kuendelea kusapoti muziki mzuri na vitu vingine vikubwa vinakuja,” amesisitiza.
Ngoma mpya ya Bill Nass ‘Sina Jambo’ ni ya tano kutoa tangu alipotoka na ngoma yake ya Raha na kufuatiwa na Ligi Ndogo, Chafu Pozi na Mazoea.
Hakuna maoni: