MCHEZAJI WAYNE ROONEY AKATWAA MSHAHARA

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemlima adhabu ya kukatwa mishahara ya wiki mbili mshambuliaji wake, Wayne Rooney kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Wayne Rooney
Makato ya fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalumu nchini humo kama sera ya klabu ya Everton ya kusaidia watu wasiojiweza.
Mahakama nchini Uingereza siku ya Jumatatu ilimuhukumu Wayne Rooney kutoendesha gari kwa miaka miwili na kufanya kazi za kijamii kwa masaa 100 baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari akiwa amelewa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.