MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA KUBADILISHA KIOO CHA KOMPYUTA YAKO
.
Leo tujikumbushe kidogo jambo muhimu sana pale unapofikia uamuzi wa kubadilisha kioo chako cha Kompyuta kilichovunjika au kushindwa kuwaka.
Dalili huwa zinajionesha katika Nyanja mbalimbali, lakini kwa leo dalili hizi.
1. Ukiweka Adapter kwenye Kompyuta yako huonesha alama ya kuwaka ishara ya kwamba umeme unaingia kwenye ubao mama, japo Kioo kinashindwa kuonesha chochote.
2. Kioo kinawaka lakini bado kinaonesha mistari mbalimbali, au unakuta mstari mmoja unagawa kioo hicho katikati dalili inayoonesha kuwa kioo kimepata hitilafu.
3. Kioo kuonesha chenga chenga au mawimbi mawimbi, japo wakati mwingine huwa ni dalili za kuwa GPU imepata hitilafu.
4. Kioo kuvunjika vipande vipande.
5. Kioo kuonesha wino unaovuja kwa ndani,
Sasa uonapo dalili hizo na unataka kubadilisha au kwenda kwa fundi unatakiwa hata wewe kwenye ufahamu wako una uwezo wa kutambua kioo ambacho unahitaji, zingatia yafuatayo pale unapotaka kubadilisha.
1. Aina/Kampuni ya Kompyuta yako, unatakiwa unapoenda kununua kioo uwe unajua kuwa kampuni uliyonunua kioo chako ni ipi? Mfano Dell, Toshiba, Acer, Asus, Hp n.k.
2. Kutambua Model ya Kompyuta yako, hii itakupa kuelewa kwa ufasaha kioo gani kinafaa kwa ajili ya Kompyuta yako. Mfano Dell Latitude e5530, n.k.
3. Kutambua Ukubwa wa Kioo, (size), kwa kawaida ukubwa wa kioo hupimwa kwa kutumia “inch”, mfano utakuta kioo kina 14inch, 17inch ,14.4 inch, 11.1inch n.k. Hivyo ni vyema ukajua ukubwa(size) ya kioo chako.
4. Aina za Vioo, Vioo hivi vimegawanyika katika makundi mawili muhimu ambayo ni
(a) Vioo vya LED (Light-Emitting Diode), hii kwa kawaida haivitumii “invertor”.
(b) Vioo vya LCD (Liquid Crystal Display), Vioo vya namna hii lazima kuwe na “invertor” vioo hivi pia kwa kawaida huwa na mwanga mkali sana.
(c) Slim. Hivi ni aina nyingine ambayo chimbuko lake ni LED, na kwa kawaida navyo vimegawanyika kwenye makundi haya
-Slim LED hivi navyo vimegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni “Normal Pin” ambayo ina Pin 40 na “Short Pin” ambayo ina Pin 30.
N.B, wakati wa kubadilisha kioo baada ya kukifungua kile ambacho kimepata hitilafu unatakiwa uwe umetoa betri maana unaweza kusababisha “Short” ya kuharibu Kompyuta yako.

Hakuna maoni: